5 Desemba 2013 - 20:30
Simba wa Afrika afaliki dunia

Ndugu Nelson Mandera baada ya muda mrefu kusumbuliwa na tatizo la mapafu na figo sasa afariki dunia, Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu ambapo alilazwa Hospitalini na baadaye kuruhusiwa kurudi nyumbani na kumfika umauti akiwa nyumbani kwake hapo mjini Pretoria.

Shirika la habari la Ahlulbayt(a.s) –ABNA: RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini aliye pambana na ubaguzi wa rangi na utabaka, muheshimiwa  Nelson Mandela amefariki dunia nchini humo akiwa na umri wa miaka 95.Nelson Mandera kuanzia mwaka 1962 mpaka mwaka 1990 alifungwa kwakosa la kupinga suala la ubaguzi wa rangi na utabaka nchini Afrika ya kusini, vitendo ambavyo vilikuwa vikifanywa na makaburu waliokuwa wakiitawala nchi hiyo ya Afrika ya kusini.Makaburu hao walihisi kuwa ndio wenye haki pekee katika nchi hiyo na kila sekta muhimu ya utumeshi wa uma wao tu ndio walikuwa wanahusika, na kila aliyekuwa anarangi nyeusi yani mzalendo wa kiafrika alikuwa akiwekwa mbalina katika sekta zote za utumishi wa Taifa hilo, mpaka kufikia hatua ya kubana sekta ya elimu kwa wazalendo wa nchi hio (kitu ambacho hata hivi sasa katika baadhi ya matifa ya kiafrika kinaonekana) , na mengineyo mengi ambayo alikuwa wakitendewa wazalendo wa Taifa, ndipo simba huyu baada ya kutafakari na kuona hali haiyo si yakibinadamu ndipo akasimama kidete katika kutetea haki za binadamu na wazalendo wa kiafrika kunako ubaguzi wa rangi na utabaka, na Mungu amtupi mja wake hatimae alifikia lengo lake hilo.Ama Taarifa za kifo chake zimetangazwa na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye alisema Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku wa Alhamisi kwamujibu wa nyakati za Afrika Kusini.Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya mapafu na figo kwa muda mrefu sana, nakupelekea kulazwa Hospitalini na baadaye kuruhusiwa kwenda nyumbani  ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.